Breaking News: Lazaro Nyalandu Ajiuzulu Ubunge na Nyadhifa Zote Ndani ya CCM
Mbunge wa
Singida Kaskazini, Lazaro Nyandu (CCM) ametangaza kujiuzulu ubunge na
nyadhifa zote ndani ya chama hicho huku akimwandikia barua spika ya
kujiuzulu.
Soma alichokisema Nyalandu.
NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za
Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA,
asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua
ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini
kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne
mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi
Sasa.
AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo
wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za
Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya
watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya
dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa
Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru
uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.
VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.
MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.
HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM .

Post a Comment