Nyalandu aangalia uwezekano wa kumhamishia Lissu Marekani
Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu ameeleza kuwa yuko Nairobi kwa mara ya pili kusubiri kupata ripoti ya matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ili waweze kumhamishia nchini Marekani kwa matibabu zaidi.
Katika ukurasa wake wa Twitter na Facebook, Nyalandu ameandika hivi, “Tumekuwa #NairobiHospital tukisubiri MADAKTARI watoe RIPOTI ya mwenendo wa MATIBABU ya Mh #TunduLissu kwa minajili ya kuwapatia MADAKTARI BINGWA wa Marekani na kuona uwezekano wa Mh #TunduLissu kupatiwa RUFAA kwa matibabu zaidi NJE., LAKINI bado KALAMU zao ni nzito kuandika RIPOTI hii siku ya tatu tangu tuahidiwe.
Binafsi, nimerudi NAIROBI tangu JANA kushiriki maandalizi ya uwezekano wa kumhamishia Mh #TunduLissu Marekani kwa ajili ya huduma yenye ubora zaidi, endapo MADAKTARI wa #NairobiHospital wangeridhia.
Kesho asubuhi nitarejea hospitalini kusikiliza kauli ya mwisho ya MADAKTARI kuhusu RIPOTI hiyo. Soma zaidi
Post a Comment