Mwenyekiti Kamati ya JPM ya Makinikia, Muhongo, Ngeleja Kitanzini
Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza jambo. Katikati ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson.
Akisoma ripoti ya kamati hiyo ambayo imekabidhiwa kwa Spika wa Bunge Job Ndugai ambaye naye ameikabidhi kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mwenyekiti wa kamati hiyo, Mussa Zungu amesema wamebaini madudu mengi.
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
“Serikali ihoji wajumbe wote wa bodi ya migodi hiyo na wote wanaohusika na ikibainika kuwa walihusika katika mapungufu waliyoyaona wachukuliwe hatua,” amesema.
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Kwanza iliyofichua upotevu mkubwa wa
mapato katika usafirishaji wa mchanga wa madini (makinikia) kwenda nje
ya nchi, Prof. Abdulkarim Mruma (kushoto) akikabidhi ripoti kwa Rais
Magufuli wakati Makamu wa Rais Samia Suluhu akishuhudia.
Amesema kuwa Mruma alikiri mbele ya kamati kuwa alishindwa kufuatilia madeni yaliyobambikwa kwa serikali ya Tanzania kwa sababu hakuwa na muda wa kusoma hivyo aliyapitisha madeni hayo kwani aliwaamini waliompelekea taarifa hizo (watendaji wa wizara).
Waziri wa Nishati na Madini wa zamani, William Ngeleja.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa kesho saa 4:30 asubuhi atamkabidhi Rais Magufuli ripoti mbili za uchunguzi wa biashara ya Almasi na Tanzanite alizokabidhiwa leo na Spika Ndugai.
Post a Comment