Makonda Akabidhi Pikipiki 10 Polisi Dar es Salaam
RC Paul Makonda akizungumza katika hafla hiyo.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo amekabidhi pikipiki 10 kwa Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ili kuimarisha usalama katika jiji hilo.Masanduku yaliyokuwa na kompyuta zilizokabidhiwa kwa jeshi la polisi.
Akimkabidhi Naibu Kamishna wa Polisi (SACP) na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, Makonda amesema ameamua kulisaidia jeshi hilo baada ya kuona lina upungufu wa vitendea kazi.Akikata utepe kuashiria kukabidhi pikipiki kwa jeshi la polisi.
Vitu vingine alivyokabidhi Makonda ni pamoja na kompyuta na baiskeli zipatazo 200.
Aidha katika hafla hiyo amewaahidi askari wa jiji lake kuwapa viwanja kwa bei nafuu ambapo alieleza kuwa tayari amekwishazungumza na kampuni ya viwanja ili kuwauzia askari kwa bei nafuu inayoanzia Sh. 5, 000 kwa kila mita za eneo badala ya bei iliyopo sasa ya Sh. 1,5000.Akipanda moja ya pikipiki alizokabidhi kwa jeshi la polisi.
“Haiingii akilini askari wanafanya kazi nzuri ya kulinda raia halafu hawana makazi bora. Nimeona niwapatie viwanja kwa gharama nafuu,” alisema Makonda.
Naye SACP Mambosasa amemshukuru Makonda kwa msaada huo na kusema jeshi hilo bado lina uhitaji mkubwa wa vitendea kazi na kuwaomba wadau waendelee kusaidia.Akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake.
Wakati huohuo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tongba ya China, Xue Chang, ambao ndiyo walitoa msaada wa pikipiki, alisema wataendelea kuisaidia serikali ya Tanzania hususani Jeshi la Polisi katika kuwapatia vifaa na hivyo na wanatarajia kujenga kiwanda cha kuunganisha pikipiki hapa nchini.
Post a Comment