Kocha wa Stars Mayanga Atangaza orodha Kikosi cha Wachezaji 21
KOCHA mkuu
wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza orodha ya kikosi cha wachezaji 21 kwa
ajili ya kujiandaa na mchezo wa kimataifa
wa kirafiki utakaokuwepo kwenye kalenda ya Fifa.
Mchezo huo unatarajia kupigwa Oktoba 7 mwaka
huu jijini Dar.
Kocha huyo
ametangaza kikosi hicho leo Septemba 23 mwaka huu mbele ya waandishi wa habari
na kusema kuwa mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Uhuru wa Dar es
Salaam.
Wachezaji
walioitwa kwenye katika kikosi hicho ni makipa Aishi Manula, Ramadhani (Simba), Ramadhan Kabwili
(Yanga), Peter Manyika (Singida United).
Mabeki ni
Gadiel Michael (Yanga), Erasto Nyoni (Simba), Boniphace Maganga (Mbao), Adeyuni
Salehe (Kagera Sugar), Kelvin Yondani (Yanga) na Salim Mbonde (Simba).
Upande
wa viungo wa Kati ni Himid Mao (Azam), Hamis Abdallah ( Sony Sugar, Kenya),Mzamiru
Yassin (Simba) na Raphael Daud (Yanga).
Viungo wa shambuliaji ni Simon Msuva (Difaa Al jadida,
Morocco), Shiza Kichuya (Simba), Morel
Ergenes (Ureno), Abdul Hilal Hasan (Tusker
FC, Kenya), Ibrahim Ajibu (Yanga) na washambuliaji watakuwa ni Mbwana Samatta
na Mbaraka Yusuph.
Post a Comment