Dondoo za Urembo: Ng’arisha miguu kwa vitu asilia
LEO kwenye safu yetu hii ya urembo tunaona jinsi ya kuipata miguu mizuri yenye ngozi inayovutia kwa kutumia vitu asilia nyumbani kwako.
1.Limao na mafuta ya mzaituni Vitu hivyo ni pamoja na limao ukichanganya na asali pamoja na mafuta ya mzaituni au ukichukua limao ukachovya kwenye asali na mafuta ya mzaituni kisha ukasugua miguu yako. Baada ya kuisugua acha kwa muda wa dakika 10 hadi 15 kisha paka mafuta au losheni unayoitumia.
2. Maziwa mgando kwa kuondoa sugu Maziwa mgando ni kwa kuondoa sugu kwenye miguu, cha kufanya chukua maziwa hayo paka kwenye miguu yako acha kwa muda wa dakika 10 hadi 15 kabla ya kuosha fanya hivyo kila unapokuwa na nafasi utaona jinsi utakavyokuwa na ngozi laini isiyokuwa na sugu.
3. Maziwa na baking soda Chukua maziwa vikombe vitatu changanya na vijiko vitatu vya baking soda. Yapashe maziwa hayo kisha changanya na baking soda ndani yake. Baada ya hapo loweka miguu yako kwenye huo mchanganyiko wako kisha kaa kwa muda wa dakika 10, osha na baada ya hapo chukua maji ya vuguvugu osha miguu hiyo kuondoa uchafu wote.
4. Mafuta ya nazi kwa miguu iliyopasuka Chukua mafuta ya nazi paka eneo lililopasuka taratibu, fanyia masaji usiku, kazi ya mafuta ya nazi ni kulainisha ngozi yako na kuifanya ilainike. Ukijaribu urembo huu utasahau kabisa kwenda kuosha miguu saluni.

Post a Comment