ad

ad

YANGA 3-2 SINGIDA UNITED ‘LIVE’ FULL TIME, UWANJA WA TAIFA


FULL TIME
Mwamuzi anamaliza mchezo, Yanga wanaibuka na ushini wa mabao 3-2, awali Yanga walikuwa nyuma kwa mabao 2-1 lakini wametoka nyuma na kupata ushindi.
Dakika ya 93: Yanga wanacharuka, wanafanya shambulizi kali, almanusura wapate bao la nne.
Mashabiki wa Yanga wanashangilia kwa nguvu.
Yanga inapata bao la tatu kupitia kwa Emmanuel Martine, alipiga shuti kali kutoka nje ya 18, mpira ukadunda na kumpoteza kipa.
Dakika ya 92: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 86: Matokeo sasa ni 2-2, furaha imerejea kwa mashabiki wa Yanga hapa uwanjani.
Tambwe anafunga, kipa anapambana kuufuata mpira lakini anashindwa kuudaka, unajaa wavuni.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Amissi Tambwe anaendaka kupiga penalti.
Dakika ya 83: Kipa wa Singida anashika miguu mshambuliaji wa Yanga aliyekuwa akielekea kufunga.
Yanga wanapata penaltiiiii
Dakika ya 80: Kenny Ally wa Singida anapewa kadi ya njano kwa kuchelewesha kucheza mpira uliokuwa umetoka.
Dakika ya 78: Inapigwa penalti anakosaaaaaaaaa.
Dakika ya 77: Penaltiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Singida wanapata penalti baada ya beki wa Yanga, Ninja kumchezea faulo mshambuliaji wa Singida.
Dakika ya 75: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Kelvin Yonda, anaingia Andrew Vincent 'Dante'.
Dakika ya 71: Inapigwa kocha lakini Yanga wanaokoa.
Dakika ya 70: Singida wanapata kona, anapiga Kiggi Makassy, walinzi wa Yanga wanaokoa inakuwa kona tena.
Dakika ya 68: Mashabiki wa Yanga wanaonyesha hawajafurahishwa na matokeo haya licha ya kuwa huu ni mchezo wa kirafiki, wapo makini kufuatilia mchezo.
Dakika ya 65: Ajibu anachukua mpira kutoka pembeni lakini anatoa pasi mapema.
Dakika ya 64: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.
Dakika ya 60: Ibrahim Ajibu anawekwa chini na Deus Kaseke wakati walipokuwa wakiwania mpira.
Dakika ya 55: Washambuliaji wa Singida wanaonekana kuwa na mbinu nyingi, wanawapa upinzani Yanga.
Dakika ya 54: Kila mara Singida wanapofanya jambo zuri mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Simba wanashangilia.
Dakika ya 50: Yanga wanatulia na kumiliki mpira kwa dakika kadhaa sasa.
Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi, Yanga wanaonakana wanatafuta bao la kusawazisha kwa nguvu
Kipindi cha pili Kimeanza
MAPUMZIKO
Dakika 45 +2 Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza, Yanga wapo nyuma kwa mabao 2-1
Dakika 43: Kipa wa Yanga, Beno Kakolanya anafanya kazi ya ziada.
Dakika ya 42: Yanga wanaonekana kutafuta bao la kusawazisha kwa nguvu zote.
Dakika ya 35: Yanga wanakosa bao la wazi kipa wa Singida United anaokoa kwa kupanchi.
Dakika 29;  Timu zote zinashambuliana kwa zamu bado Yanga 1- 2 Singida United
Dakika 27: Singida United wanapiga faulo kuelekea lango la Yanga, Ynaga wanaokoa.
Goooooooooooooo Singida United wanapata bao la pili
Dakika ya 19: Bado matokeo ni 1-1 timu zote zinashambuliana kwa zamu  Kelvin Yondani anafanya kazi kuwadhibiti washambiliaji wa Singida United.
Dakika ya 14; Singida United wanakosa bao la wazi kabisa, Yondani anatoa nje.
Dakika 13; Yanga wanamiliki mpira na kufanya mashambulizi mara kwa mara
Dakika ya 6: Yanga 1-1 Singida united mchezo upo sepeed sana wanashambuliana kwa kazi
Sigida  United wamekosa penalti baada ya mchezaji wao kuangushwa ndani ya bosi. Singida United wamepiga penalti wamekosa.
KIKOSI:
1. Youthe Rostand
2. Juma Abdul 
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Abdallah Shaibu 'Ninja'
6. Thaban Kamusoko
7. Burhani Yahya
8. Raphael Daud 
9. Amiss Tambwe
10. Donald Ngoma 
11. Ibrahim Ajibu

SUB:
Beno Kakolanya
Hassan Kessy
Nadir Haroub
Andre Vicent
Juma Mahadhi
Yusuf Mhilu
Edward Martin

No comments

Powered by Blogger.