Waziri Lukuvi Azindua Mji Wa Kisasa Arusha

Na Nahmoud Ahmad Arusha
Waziri
wa ardhi , nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi amewaagiza
viongozi wa halmashauri na majiji nchini kuharakisha utoaji wa vibali
vya ujenzi na kuachana na urasimu unaosababisha kuwepo kwa ujenzi holela
.
Lukuvi aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa nyumba kumi za mfano za mradi wa mji wa kisasa wa Safari City zilizopo Mateves sambamba na kutoa hati miliki kwa wanunuzi 100 wa kwanza wa viwanja zinazotekelezwa na shirika la nyumba la taifa (NHC) .
Alisema
kuwa kumekuwepo na ucheleweshaji mkubwa wa vibali vya ujenzi
unaosababishwa na wahusika wenyewe na hivyo kupelekea wananchi hao
kujenga kiholela kutokana na wananchi hao kuchoka kusubiri.
Aidha
kufuatia hali hiyo alimwagiza mkuu wa mkoa wa arusha Mrisho Gambo
kufanya ukaguzi wa mafaili ya vibali vya ujenzi na kuweza kugundua idadi
ya watu ambao hawajapatiwa vibali vyao mpaka sasa hivi.
“Unajua
idadi kubwa ya wananchi wanaojenga kiholela sio kwamba wamevunja sheria
bali wanafanya hivyo kwa ajili ya ucheleweshaji wa vibali kwa hiyo
hatua hiyo inasababisha pia kuchelewa kutoana na kusubiri kwa muda mrefu
bila kupata jibu lolote”aliongeza Lukuvi.
Awali
mkurugenzi mkuu wa shirika la nyumba la taifa Nehemia Mchechu alisema
kuwa mradi huo wa kitovu cha mji wa kisasa wa safari city jijini hapa
una ukubwa wa hekari 559.4 na ni sehemu ya miji iliyopangiliwa kitaalamu
na kwa kuzingatia sheria za mipango miji.
“Mradi
huu ulibuniwa na shirika la nyumba kwa lengo la kupunguza uhaba wa
makazi kwenye jiji hili ambapo tumetenga maeneo kwa ajili ya
waendelezaji kujenga sehemu za biashara,burudani ,utalii,hospitali,
elimu,huduma za kijamii kama vile polisi,na zimamoto lakini pia yapo
maeneo ya wazi kwa ajili ya michezo na mapumziko”alisema Msechu.
Aidha
Mchechu aliziomba taasisi kuunga mkono maagizo aliyoyatoa raisi kwa
halmashauri na taasisi zinazohusika kuhakikisha kuwa zinaweka
miundombinu yote muhimu katika maeneo yanayohitajika kuendelezwa na NHC
ili kuweza kupunguza gharama za nyumba zinazojengwa


Post a Comment