Usain Bolt Aumia Mbio za Kupeana Vijiti IAAF
Usain Bolt jana
aliumia na kushindwa kumaliza mbio zake za mwisho za ubingwa wa dunia jijini
London, na mwanariadha mwenzake Yohan Blake anasema huenda kucheleweshwa kwa
mbio hizo kulimwathiri
Bolt alipata
mkakamao wa misuli na kulazimika kuondoka uwanjani alipokuwa akikimbia mbio za
kupokezana vijiti za 4x100m ambazo timu ya Uingereza ilishinda.
Yohan Blake alisema:
"Mbio zilicheleweshwa dakika 10, tuliwekwa tukisubiri kwa dakika 40.
Ilitushangaza sana.”
Bolt alikuwa
ametumaini angemaliza maisha yake ya ukimbiaji kwa kushinda dhahabu mbili
mashindano hayo ya London lakini ameondoka na nishani ya shaba pekee aliyoshinda
kwenye mbio za mita 100 wikendi iliyopita.
Sekunde
chache baada yake kupokezwa kijiti awamu ya mwisho ya mbio hizo, alishikwa
msuli na kuanguka.
Daktari wa
timu ya Jamaica Kevin Jones amethibitisha kwamba Bolt alipatwa na mkakamao wa
misuli ya mguu wake wa kushoto.
"Tulikaa
tukipasha misuli na kusubiri, kisha tunapasha misuli tena na kusubiri. Nadhani
hilo lilituathiri,” alisema Blake.
Post a Comment