UHAMIAJI YATHIBITISHA KUWA WALLACE KARIA NI MTANZANIA, BAADA YA KUWEKEWA PINGAMIZI
Mgombea wa urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, ambaye alikuwa katika wakati mgumu juu ya uraia wake, sasa imethibitka wazi kuwa ni Mtanzania.
Hilo limesemwa leo na Idara ya Uhamiaji Tanzania.
Karia ambaye kwa sasa anakaimu nafasi ya urais katika shirikisho hilo, aliwekewa pingamizi na mgombea mwenzake kwenye nafasi hiyo, Iman Madega akidai kwamba si raia wa Tanzania kabla ya uhamiaji kufanya uchunguzi ikiwemo kuchukua vipimo vya vinasaba (DNA) vya mgombea huyo.
Msemaji Mkuu wa Uhamiaji, Mrakibu Ally Mtanda asema wamechunguza kwa umakini na kujiridhisha kuwa mgombea huyo alizaliwa Tanzania huku baba yake akiwa ni raia wa Somalia.
“Kutokana na msingi huo Karia alikuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu 5(1) na (2) cha sheria ya uraia ya Tanzania sura ya 357 (Rejeo la 2002 na kanuni zake,” alisema Mtanda.
Post a Comment