Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) laonywa jinsi lilivyomaliza mgogoro wa Makonda na Clouds
Kufuatia
maoni ya baadhii ya watu mbalimbali na waandishi wa habari kutoridhika
na maamuzi ya Jukwaa la Wahariri (TEF), viongozi wamepewa onyo la
kutorudia makosa baada ya kukiri.
Katika
mkutano mkuu uliofanyika Agosti 13, viongozi hao walikiri kuitisha
mkutano na waandishi wa habari Agosti 9 bila ya kupata idhini.
Hatua hiyo ilisababisha kujengeka kwa taswira mbaya kiuwajibikaji, kanuni na utaratibu.
Katika
taarifa ya Mwenyekiti Maalum wa TEF, Walace Mauggo imeeleza kuwa jukwaa
kwa kauli moja limetoa onyo kwa viongozi wake kutorudia yale ambayo
yamejitokeza.
“Baada
ya kutafakari na kutathmini mwenendo wa mkutano huo, jukwaa lilobaini
kuwepo kwa kasoro kubwa wakati wa kurejesha mahusiano wa kikazi na
kiongozi ambaye habari zake zilizuiwa kuripotiwa kwa takribani miezi
mitano,” imeeleza taarifa hiyo.
Pia
wametakiwa kuhakikisha kunapotokea masuala makubwa kama hayo ambayo
yashafanyiwa maamuzi na mkutano mkuu na taasisi nyingine za habari
yanarudiswa maamuzi kwa wanachama kabla ya hatua za mwisho.
Mauggo
ameeleza kuwa TEF haitasita kuchukua hatua kwa kiongozi au mtu yoyote
atakayeonekana kutishia usalama wa wanahabari, uhuru wa uhariri na
vyombo vya habari.
Post a Comment