Jinsi Ya Kupika Chapati Laini Za Kusukuma, Maitaji Yote Yapo Hapa
Mahitaji
-Unga wa ngano nusu kilo.
-Siagi vijiko 2.
-Yai moja.
-Chumvi kiasi.
-Hiliki kama unapenda maana wapo ambao hawapendi.
-Maji ya uvuguvugu kwa ajili ya kukandia.
-Mafuta ya kupikia.
Jinsi ya kuandaa
Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri.
Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri weka yale maji ya uvuguvugu kidogo kidogo huku ukikanda, ukande mpaka uhakikishe haunati ila umekuwa laini.
Kukanda huko kutumie kama dakika 15 hivi ndiyo utalainika vizuri, ukimaliza katakata madonge kulingana na chapati unazotaka, hakikisha saizi inakuwa sawa kwa yote.
Ukimaliza, sukuma donge moja baada ya jingine. Ukishasukuma paka mafuta kisha weka donge pembeni mafuta yale yape nafasi ya kuingia ili kuifanya chapati iwe laini zaidi.
Ukishamaliza madonge yote chukua la kwanza sukuma anza kupika, pika chapati zako kulingana na jinsi ulivyokuwa ukizipaka mafuta moja baada ya nyingine.
Post a Comment