ISHU YA HANS POPPE KUPEWA KAZI YA KUANDAA SUPU YA YANGA, IPO HIVI
HARAKATI za mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu zinaendelea, bosi wa Simba, Zacharia Hans Poppe amepewa jukumu la kuhakikisha Yanga wanapata kichapo.
Hans Poppe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba amepewa majukumu hayo lakini siyo ambayo yanahusiana na mambo ya ufundi wa ndani ya uwanja yanayofanywa na benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Mcameroon, Joseph Omog.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameliambia Championi Ijumaa kuwa: “Hatutaki mchezo kabisa safari hii, tunachotaka ni ushindi kwa hiyo tumeamua kumkabidhi komandoo wetu, Zacharia Hans Poppe majukumu maalumu ya kufanya ili tuweze kuibuka na ushindi.
“Kila mtu ndani ya Simba anajua kuwa Hans Poppe siyo mtu wa mchezomchezo kwa hiyo tunaamini kuwa atawaandalia Yanga supu ya mawe siku hiyo,” alisema Manara.
CHANZO: GPL
Post a Comment