FAIZA ALLY AJIFUNGUA KIDUME
MFANYABIASHARA na muigizaji wa Bongo muvi ambaye pia ni mwanamitindo asiyekaukiwa vituko, Faiza Ally, amejifungua mtoto wa kiume na amempa jina la Lil Junior.
Faiza ambaye ni mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu, amejifungua leo katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam, ambapo amethibitisha taarifa hizi kupitia ukurasa wake wa Instagram:
“Asanteni sana ndugu zangu Watanzania nimeishiwa na maneno kwa mapenzi yenu. Najiona kila kona kwenye kurasa mbalimbali za marafiki, umbea, habari yaani najihisi kupendwa.
“Na nimezidi kutambua kuwa uwepo wangu upo, naomba niwaambie nawapenda sana, natambua uwepo wenu wote, natamani ningejibu kila comment , nipite kila kurasa, nijibu msg zote DM na WhatsApp ndiyo usipime yote hayo ni mapenzi, najisikia baraka kwa kweli, furaha yangu inazidi mara dufu ALHAMDULILLAH.
“Nawatakia kila la kheri na baraka tele kwenu, wanaotafuta watoto Mwenyezi Mungu awajaalie kila la kheri mpate, na waliopata INSHAALLAH, Mwenyezi Mungu awatunzie wawe watoto wenye baraka kwenu AMEN YARAB. Nawapenda Watanzania, naipenda Tanzania, Mungu tubariki sisi na vizazi vyetu AMEN.”
Post a Comment