Amanda Afunguka Bwana Kumpiga Stop Kuigiza
MREMBO
mwenye shepu yake Bongo Movies, Amanda Posh amepangua uvumi uliozagaa
mtaani kuwa, amezuiwa kuigiza na mchumba wake kwa kusema si kweli.
Amanda
alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akipiga stori
na
mwanahabari wetu ambaye alimbananisha swali kuhusu ukimya wake kwenye gemu na
madai hayo ya kuzuiwa kuigiza.
“Bwana
hawezi kunizuia kuigiza sema nilikuwa tu bize na masuala yangu binafsi ya
kibiashara ndio maana kwa zaidi mwaka sasa nimekuwa kimya kwenye sanaa, ila
nitarudi tu maana sanaa ndio kila kitu kwangu,” alisema Amanda.
Post a Comment