NGOMA YUPO FITI 100% ATUMA SALAMU
S TRAIKA wa Yanga, Donald Ngoma ametuma salamu kwa mashabiki wa timu hiyo akisema kuwa yupo fiti asilimia 100 na Jumanne ya wiki ijayo atatua nchini.
Ngoma raia wa Zimbabwe, alikuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi minne akiuguza majeraha ya goti na aliwahi kwenda kutibiwa Afrika Kusini. Mara baada ya kupatiwa matibabu hayo alikaa nje ya uwanja akifanya mazoezi mepesi kabla ya wiki iliyopita madaktari wake kumruhusu kuanza mazoezi baada ya kufanyiwa vipimo vya mwisho.
Akizungumza Ofisa Habari Msaidizi wa Yanga, Godlisten Chicharito alisema, amewasiliana na Ngoma na amewaondoa hofu mashabiki kwa kusema yupo fiti kwa ajili ya kuitumikia timu yake.
Chicharito alisema: “Ngoma msimu uliopita hakutoa mchango mkubwa katika ubingwa tuliochukua kutokana na majeraha ya goti, kitendo cha yeye kukaa nje na kutotoa mchango katika timu kumemfanyia ajisikie vibaya.
“Sasa ameahidi kuipambania timu yake ya Yanga kwa asilimia kubwa ili ichukue ubingwa wa ligi kuu na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa. “Ameniambia anakuja nchini Jumanne ya wiki ijayo na moja kwa moja ataanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu,” alisema Chicharito.

Post a Comment