Nandy Afunguka baada ya kudaiwa kuwa mapenzini na Billinass
Kupitia XXL ya Clouds FM leo July 14, 2017 Nandy amesema hawako mapenzini na Billnass bali yupo kwenye mahusiano na mu mwingine ambaye hawezi kumuweka hadharani.
>>>”Nikitoka hapa nahisi huko nakoenda naenda kuachwa kwa sababu nina mahusiano yangu sitoki na Billinass. Kwa kweli mmeyavunja mahusiano yangu. Tuwe Serious kwenye hili maana nisingependa mashabiki wangu waone hivyo. Sitoki na Billinass hatuna mahusiano.
“Mashabiki wanavyoona wanaongea, hatuna hata ukaribu. Haiwezi kutokea, itakuwa ni ngumu kwa sababu mimi nina uhusiano, nina mpenzi wangu yupo japo siwezi kumuweka Public. – Nandy.
Post a Comment