Msuva: Nimetua Salama Morocco
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva.
WINGA wa Yanga, Simon Msuva amefika salama nchini Morocco na tayari kupimwa afya kisha akimaliza hapo anatarajiwa kusaini mkataba leo Ijumaa.
Msuva aliondoka nchini juzi Jumatano saa tatu kamili usiku na kuelekea Morocco kwa ajili ya kwenda kujiunga katika Klabu ya Difaa El Jadida iliyokuwa inamuwania vikali.
Akifanikiwa vipimo hivyo basi atakuwa ameitajirisha timu yake ya Yanga anayoichezea kwa kumuuza kutokana na kuwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea Jangwani.
Akizungumza na Championi Ijumaa, mara baada ya kutua nchini huko, Msuva alisema anawashukuru mashabiki wa Yanga na Watanzania wote kwa kumuombea safari yake na kufika salama.
"Nawashukuru Watanzania wote wakiwemo mashabiki wa Yanga walioonyesha upendo juu yangu na kunipa baraka zote na kufanikiwa kufika salama hapa Morocco.
"Nimefika huku majira ya saa tano asubuhi na kwa saa za huko nyumbani ni saa saba na robo, hivyo baada ya kufika nilipokewa na viongozi wa timu iliyoniita huku.
"Nimepewa muda wa mapumziko siku ya leo na kesho (leo) ninatarajia kufanyiwa vipimo na baada ya hapo, basi nitasaini mkataba," alisema Msuva.
TIMU za mpira wa kikapu za Mchenga BBall Stars na Young Dribblers, kesho Jumamosi zitakutana katika nusu fainali ya pili ya mashindano ya Sprite BBall Kings kwenye Viwanja vya Don Bosco.
Nusu fainali hiyo ya pili inachezwa huku Mchenga wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa pointi 116- 69 ilioupata katika nusu fainali ya kwanza hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Masoko ya EATV ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo, Roy Mbowe, ushindani umeongezeka katika Sprite BBall Kings ambapo bingwa atapata Sh milioni 10.
CHANZO: CHAMPIONI

Post a Comment