MAMA ALIYEKUTWA UCHI BARABARANI AZUA MJADALA
TUKIO la
mama ambaye jina lake halikupatikana mara moja kukutwa ameketi katikati ya
barabara akiwa uchi wa mnyama limezua tafrani na mjadala mkali kufuatia
mazingira ya tukio zima huku maswali yakiwa mengi kuliko uhalisia.
Kisanga
hicho kilichozua taharuki na zogo kutoka kwa watu, kilijiri jana asubuhi maeno
ya Banana-Ukonga jijini Dar hali
iliyopelekea kusimama kwa shughuli za kijamii kwa muda wa dakika kadhaa.
MAZINGIRA
YA TUKIO
Mapema
asubuhi, wakati watu wakianza ‘mishemishe’ za kuikaribisha siku mpya ndipo mama
huyo alionekana ameketi katikati ya barabara, akiwa mtupu na pembeni kukiwa na
ungo pamoja na mkoba, jambao lililovuta hisia za wengi na kulazimika kusogea
karibu na eneo hilo kushuhudia kwa ukaribu ili kubaini kilichojiri.
Alizidi
kudaiwa kuwa, mama huyo alisikika akizungumza maneno yasiyoeleweka huku akiwa
na kiwewe akijaribu kutafuta namna ya kujisitiri kuondokana na aibu. Kutokana
na hali hiyo, baadhi ya akina mama waliingiwa na moyo wa huruma kwa mwanamke
mwenzao na kujitolea mavazi (khanga) na
kumsitiri ingawa wengine hususana wanaume walisikika wakizomea na kushangilik
huku wakimuita majina yenye tafsiri mbaya.
MJADALA
ULIOZUKA
Katika
eneo la tukio, yapo maswali makubwa matatu yaliyozua mjadala ambayo
yalichangiwa na mazingira husika.
“Mbona
mwanamke mwenyewe anaonekana mstaarabu wa kutoendana kabisa na mazingira haya?
Lakini pia kama ni mchawi au muwanga mbona anaongea wakati ilivyo kawaida kama
mchawi akinaswa akifanya uchawi wake huwa hawaongei hadi ‘wagutuliwe’ tofauti
na alivyoonekana mwanzo akizungumza mwenyewe, lakini pia mbona kuna mkoba, mchawi huwa na
mkoba kweli?” hayo ni baadhi ya maswali yaliyosikika kutoka kwa watu waliokuwa
eneo la tukio, huku yakizua mjadala na sintofahamu yenye fumbo zito.
Post a Comment