FT: SportPesa Cup; Everton 2-1 Gor Mahia
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 6 za nyongeza.
Dakika ya 87: Gor Mahia wanarudi nyuma kuzuia.Dakika ya 82: Everton wanapata bao la pili kupitia kwa Kieran Dowell ambaye anawatoka walinzi wa Gor Mahia na kupiga shutli ambalo limejaa wavuni moja kwa moja.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 81: Shambulizi lingine kali langoni mwa Gor Mahia lakini mpira unagonga mwamba na kutoka nje.
Dakika ya 76: Everton wanapata kona, inapigwa ndegu na kupigwa kichwa lakini inatoka nje inakuwa goal kick.
Dakika ya 70: Kasi ya mchezo imeongezeka upande wa Everton, wanafanya mshambulizi mara kadhaa.
Dakika ya 65: Everton wanafanya shambulizi kali lakini wanakosa umakini mpira unatoka nje.
Dakika ya 55: Kumbuka matokeo bado ni 1-1, Kocha wa Everton, Dylan Kerr anatoa maelekezo mara kadhaa kwa wachezaji wake.
Dakika ya 53: Kasi inaendelea na sasa Everton wanaonekana kujipanga zaidi kwa kutengeneza nafasi kadhaa.
Dakika ya 49: Kasi ya mchezo inaendelea lakini siyo kubwa kama ilivyokuwa kipinsi cha kwanza.
Kipindi cha pili kimeanza.
MAPUMZIKO
Kipindi cha kwanza kimekamilika.
Dakika ya 45: Mwamuzi anaweza kukamilisha kipindi cha kwanza muda wowote kuanzia sasa.
Matokeo ni 1-1.
Dakika ya 37: Jacques Tuyisenge anaisawazishia bao Gor Mahia kwa kuunganisha mpira wa kona, bao zuri kabisa hapa kwenye Uwanja wa Taifa.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!
Dakika ya 36: Mchezo unaendelea, kasi inaongezeka.
Dakika ya 35: Wayne Rooney anaipatia Everton bao la kwanza, alipiga shuti kali kutoka nje ya eneo la 18 na kujaa wavuni baada ya kipa kuwia ametoka kwa mbele kidogo ya lango lake.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Mashabiki ni wengi uwanjani hapa.
Dakika ya 22: Mchezo umesimama kuna mchezaji wa Gor Mahia yupo chini.
Dakika ya 20: Timu zote zote zinasomana kwa zamu na zionashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 15: Everton wanapata faulo, anapiga Rooney lakini kipa anadaka.
Dakika ya 10: Kila Rooney anaposhika mpira anashangiliwa.
Dakika ya 5: Mashabiki ni wengi na wale wanaomshambikia Rooney ni wengi pia uwanjani hapa.
Mwamuzi Mujuni Nkono anaanzisha mchezo.
Muda wowote kuanzia sas amchezo huu wa kirafiki utaanza hapa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Post a Comment