Adebayor Anaitandika Tu Familia Yake!
Mchezaji wa Basaksehir ya Uturuki, Emmanuel Adebayor.[/caption]
KATIKA maisha kuna mambo mengi ambayo kwako yanaweza kuwa ni ya ajabu lakini kwa mtu mwingine, au jamii nyingine hicho unachokiona cha ajabu kwao ni cha kawaida na ndiyo maisha yao au maisha ya mtu fulani.
Hali hiyo inatokana na tamaduni, tamaduni ya kuzungumza ukweli hata kama ni mchungu ni kitu ambacho wanadamu wengi kinawasumbua.
Mara nyingi imetokea mtu ameumizwa kihisia au kivitendo na mtu ambaye anamheshimu au amemzidi umri au kunaweza kuwa na ukaribu mwingine wowote kisha akashindwa kuzungumza hadharani matokeo yake akafa na ‘tai shingoni’ yaani bila kueleza hisia zake.
Wapo ambao ni kawaida yao kueleza hisia zao hata kama wanajua wakifanya hivyo wanaweza kuwa wanakosea au wanaonekana wa ajabu kwa wengine, hivyo ndivyo ilivyo kwa Emmanuel Adebayor.
Unakumbuka lile sakata lake na familia yake? Sasa habari ni kuwa siyo kwamba limeisha, lipo na kinachoendelea kwa sasa ni kila upande kuishi ‘kimpango wake’ akiwemo mama yake mzazi wa straika huyo ambaye kwa sasa anaichezea Basaksehir ya Uturuki.
Emmanuel Adebayor akiongea na refa (hayupo pichani).Adebayor aliwahi kunukuliwa akisema kuwa familia yake ilichangia kwa kiasi kikubwa kutaka kumrudisha nyuma kwa kuwa walichokuwa wakijali kwake ni utajiri wake na wala hawakumjali yeye binafsi ndiyo maana licha ya kudai kuwafanyia mengi mazuri bado hawakumthamini.
Alisema kuwa baada ya kutoka kwenye umasikini, akapambana kucheza soka mwisho akawa mchezaji mkubwa nchini England, akilipwa mshahara mkubwa, familia yake ikawa inatumia fedha zake hovyo bila kujali kuwa yeye anazitafuta kwa nguvu kubwa awapo uwanjani.
Wiki hii ameendelea kuonyesha hisia zake juu ya familia yake kwa kudai ilichangia yeye kutopata dili la kuendelea kuichezea Real Madrid mwaka 2011 baada ya kuwa klabuni hapo kwa mkopo.
Straika huyo wa zamani wa Arsenal, alijiunga na Real Madrid akitokea Manchester City na kufunga mabao matano katika mechi 14 za La Liga alizocheza chini ya Kocha Jose Mourinho, baada ya msimu kumalizika hakuongezewa mkataba wa kuendelea kucheza hapo.
Wakati anaachwa na Madrid kwa kutoongezewa mkataba, ilielezwa kuwa dau lake la usajili euro milioni 16 lilikuwa kubwa lakini mchezaji huyo ameitaja sababu nyingine ya kukwama kwa dili hilo.
Adebayor ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 33 anasema kuwa akiwa Madrid, kaka yake alituma barua ya kikazi klabuni hapo akiwasisitiza kutomsajili.
[caption id="attachment_156380" align="aligncenter" width="778"] Akiwa kwenye pozi.[/caption]“Ilikuwa kipindi cha mpito na kigumu, nilichokizungumza kipindi kile sijakijutia na ninaona nilikuwa sahihi, kwenda hadharani kuzungumza juu ya hicho kitu kilinipa amani ya moyo,” anasema na kuongeza:
“Kuna watu waliniambia nilitakiwa niyaweke moyoni hayo mambo kwa kuwa ni ya kifamilia lakini binafsi nilipambana kuichezea Real Madrid ili nibaki lakini marehemu kaka yangu hakutaka hilo.
“Alituma barua rasmi kutoka kwenye familia yangu na kuiambia klabu kuwa isinisajili.
“Siyo kwamba hiyo ilikuwa sababu kubwa ya Madrid kutoendelea kuwa na mimi lakini ilichangia, hata kama ni kwa asilimia 10 lakini ni nyingi.”
Adebayor anasema kuwa bado hana uhusiano mzuri na familia yake ambayo hata alipokuwa majeruhi hakuna aliyejali kuhusu afya yake, badala yake walimuulizia kuhusu fedha.
Staa huyo raia wa Togo amekuwa na tabia ya kuonyesha kujiamini bila kujali nani ambaye anataka kumvuruga, inakumbukwa kuwa akiwa Arsenal aliwahi kukwaruzana na wachezaji wenzake kadhaa na akaonyesha jeuri ya kuwajibu bila kujali kuwa walikuwa maarufu kuliko yeye awali.
Hata alipoondoka na kutua Manchester City alionyesha kujiamini na hakujali ukubwa wa klabu aliyotoka, pia mara kadhaa amewahi kukwaruzana na makocha ambao walionyesha tabia za kutaka wanyenyekewe.
Mkataba ambao aliupata wakati anasajiliwa na Man City ulichangia kumfanya apate fedha nyingi, ambapo anasema aliwajengea nyumba na kuwanunulia magari ndugu zake lakini hiyo wakaona haitoshi wakataka awe anawalipa mishahara bila kufanya kazi yoyote.
Ilipotokea amekosa timu ya kuichezea hakuwa na papara ya kutafuta timu kwa kuwa aliamini bado ana uwezo wa juu na anaweza kucheza kwa muda mrefu, ndiyo maana ligi iliendelea huku yeye akifanya mazoezi na kula bata.
Mkataba wake wa sasa ndani ya Basaksehir unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao wa 2017-18.
Kwa sasa Adebayor ameshaoa na ana binti anayejulikana kwa jina la Kendra. Aliwahi kusema kuwa safari yake ya soka ilianzia mtaani nchini Togo, huko alionwa na wakala ambaye alimchukua na kumpeleka kwenye timu ya Metz ya Ufaransa mwaka 1999, kilichofuata ni historia.
(ISTANBUL, Uturuki | Championi Ijumaa)

Post a Comment