Vitu saba vilivyofanya wabunge wasimame na kupiga makofi bajeti ikisomwa
Kutoka Bungeni Dodoma jana June 8, 2017 Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Phillip Mpango aliwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18, hivi ni baadhi ya vitu ambavyo wakati vinasomwa viliwafanya wabunge wapige makofi kwa wingi na hata kusimama wakishangilia.
1.Waziri ametangaza kufuta ada ya mwaka ya magari iliyokuwa inalipwa hata kwa magari ambayo hayatumiki badala ada hiyo italipwa kwa magari yanayotembea tu , Waziri amesema wamefuta ada hiyo ili ilipwe mara moja gari linaposajiliwa baada ya hapo liendelee kulipiwa kwenye ushuru wa bidhaa za petrol na diesel aidha Serikali imetoa msamaha wa kodi, riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote ya ada hiyo.
2.Kusamehe ongezeko la thamani kwenye vyakula vya mifugo vinavyotengenezwa hapa nchini ili kupunguza gharama za kununua vyakula hivyo kwa wafugaji.
3.Waziri amependekeza kutoza kodi ya ongezeko la thamani kwa kiwango cha asilimia 0 katika huduma zinazotolewa kwenye usafirishaji wa bidhaa na mizigo nje ya nchi ili kuifanya Tanzania iwe njia bora ya kupitisha bidhaa zinazotoka nje ya nchi kwenda nchi zingine.
4.Kingine alichokisema Waziri Mpango ni kuwa Serikali haitaruhusu usafirishaji wa madini kutoka migodini na kupeleka moja kwa moja nje ya nchi aidha Serikali itaanzisha maeneo maalum latika viwanja vya kimataifa, migodini, bandarini, mipakani ambapo madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali cha kusafirisha madini hayo ambacho kitatozwa ada ya 1% ya thamani ya madini hayo.
5.Mtu anayesafirisha mazao yake kutoka halmashauri moja hadi nyingine yasiyozidi tani moja asitozwe ushuru
6.Kutoza ushuru wa forodha kwa kiwango kwa asilimia 0 badala ya 25% kwenye malighafi na vifaa vinavyoagizwa nje ya nchi kwa ajili ya kuunganisha na kutengeneza vifaa ambavyo ni mahususi kwa ajili ya matumizi ya walemavu
7. Kufutwa kwa Ushuru wa mabango yanayoelekeza mahali huduma za jamii hususani shule, hospitali na zahanati zinapopatikana
Post a Comment