Staa mwenye mvuto wa kipekee wa Bongo Muvi, Irene Uwoya.
STAA mwenye mvuto wa kipekee wa Bongo Muvi, Irene Uwoyaamefunguka kuwa anachukizwa na ishu ya kuulizwa lini ataongeza mototo mwingine baada ya mtoto wake wa kwanza, Krish huku kukiwa na mastaa wengine ambao hawana hata mtoto wa kusingiziwa.
Akizungumza na 3 Tamu, Uwoyaalisema
kuwa, hata kama yeye hatazaa tena, lakini ishu hiyo haita msumbua kwa
sababu tayari Mungu, amembariki hivyo jambo la yeye kutoongeza mtoto
mwingine halimuhusu kabisa. “ Nashangaa sana mtu anakwambia Krish
amekua mkubwa anahitaji mdogo wake, ni jambo la kushangaza kwa sababu
ambao kuna mastaa wengine umri unayoyoma lakini hawana hata mtoto wa
kusingiziwa,” alisema Uwoya.
Post a Comment