USAJILI WA WACHEZAJI 10 ULIOFUNIKA LIGI KUU BARA MSIMU WA 2016/17
Licha ya wingi wa nyota wapya msimu uliopita ila ni wachezaji wachache pekee ndiyo walifanikiwa kufikia angalau nusu ya matarajio.
Zaidi ya milioni 500 zilitumika msimu uliopita kwenye usajili wa wachezaji nyota kutoka sehemu mbalimbali Afrika walifanikiwa kujiunga na Ligi Kuu Bara kwa msimu ulioisha.
Licha ya wingi wa nyota wapya msimu uliopita ila ni wachezaji wachache pekee ndiyo walifanikiwa kufikia angalau nusu ya matarajio.
Usajili baadhi kwa msimu uliopita ndiyo ulifanya vizuri na kurudisha thamani japo kidogo kwa klabu yake.
Huu ni usajili wa wachezaji kumi uliofanya vizuri msimu uliopita wa 2016/2017:
10. Stephan Kingue
Kiungo mkabaji wa Azam FC, Kingue amefanya vizuri sana msimu ulioisha kwa kujaribu kumpungunzia majukumu Himid Mao, usajili huu ni bora kwa Azam kwenye eneo la kiungo.
9. Kwasi Asante
Mlinzi kutoka Ghana anayekipiga Mbao FC, mlinzi huyo amefanya kazi kubwa msimu uliopita na kuiwezesha Mbao kusalia Ligi Kuu na kucheza fainali ya Kombe la FA.
8. Mzamiru Yasin
Kiungo mshambuliaji wa Simba, alisajiliwa kutoka Mtibwa Sugar, msimu uliomalizika amefanikiwa kutikisa nyavu mara nane, ni mabao mengi kuliko kiungo yeyote Ligi Kuu msimu uliomalizika.
7. Juma Kaseja
Alitua Kagera Sugar wakati wa dirisha dogo akitokea Mbeya City, licha kucheza nusu msimu ila ulitosha kumfanya kuwa mmoja wa makipa bora msimu uliomalizika.
6. Yusuph Ndikumana
Amesajiliwa na Mbao FC akitokea kwao Burundi, mlinzi huyo tayari ameshaanza kuwindwa na klabu kubwa baada ya kuwa na kiwango bora kwa kuiwezesha klabu yake kusalia Ligi Kuu na kucheza fainali ya Kombe la FA.
5. Method Mwanjali
Mlinzi mkongwe wa kati wa Simba, Mwanjale ni mmoja wa usajili bora msimu uliopita kwa kuifanya Simba kuwa na ulinzi bora kwa kuruhusu mabao machache.
4. Youthe Rostand
Licha ya klabu yake ya Afrika Lyon kushuka daraja ila Mcameroon huyo alifanya kazi yake vizuri, Simba na Yanga tayari wameanza kuulizia huduma yake baada ya kuvutiwa na uwezo wake.
3. Yakubu Mohammed
Kwa muda mfupi ndani ya Azam FC, amefanikiwa kuziba pengo la beki Pascal Wawa kwa zaidi ya asilimia 60, Mghana huyo ni moja ya usajili bora msimu uliomalizika.
2. Shiza Kichuya
Amefanikiwa kufunga magoli 15 na kutoa pasi za magoli zaidi ya 10 kwenye Ligi msimu ulioisha, tangu ajiunge na Simba akitokea Mtibwa amefanikiwa kurudisha thamani yake klabuni.
1. Obrey Chirwa
Alijiunga Yanga akitokea FC Platnumz ya Zimbabwe, alianza msimu kwa kusuasua, Chirwa amefanikiwa kumaliza na mabao 12 na kuiwezesha timu yake kutetea taji kwa msimu wa tatu mfululizo.
CHANZO: GOAL.COM
Post a Comment