Uamuzi wa ACT Wazalendo kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
Kufuatia
uteuzi huu na kwa kuzingatia unyeti na majukumu ya Mkuu wa Mkoa, Kamati
ya Uongozi ya chama itakutana kesho tarehe 07 Juni 2016 kutafakari
pamoja na mambo mengine, namna ambavyo Mama Anna Mghwira atatekeleza
wajibu wake wa uenyekiti wa chama na majukumu yake mapya.
Chama kinatoa wito Kwa wanachama wote kuendelea na utulivu wakati vikao vya Chama vinachukua hatua stahiki kuhusu jambo hili.
Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma,
ACT Wazalendo.
Imetolewa leo tarehe 06 Juni 2017
Post a Comment