Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Tano na Vyuo Vya Ufundi 2017
Kutazama majina ya wanafunzi na shule walizochaguliwa ===> Bofya hapa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017
huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa.
Simbachawene ametoa kauli hiyo leo
mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na kusema kuwa
ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na
matokeo ya mwaka 2015.
Waziri amedai kati ya wanafunzi
96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019
tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.
Waziri Simbachawene amesema kuwa
jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule
kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni
47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa
daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya
watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.
Simbachawene alisema kutokana na
mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla
ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato
cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi
kama vilivyoaibishwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia ambapo
kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi
ya elimu ya watu wazima.
Aidha amewataka wanafunzi wote
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili kwa wakati katika
shule walizopangiwa July 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na mabadiliko
ya shule walizopangiwa.
“Na kama kuna mwanafunzi ambaye
hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 14 nafasi yake
itachukuliwa na mtu mwingine,” alisema Simbachawene.
Post a Comment