NYAMLANI AINGIA KUGOMBEA URAIS TFF TENA, ANACHUKUA FOMU KESHO
Aliyewahi
kuwa Makamu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani
Nyamlani, ameamua kugombea tena urais wa shirikisho hilo.
Taarifa
za uhakika kutoka kwa rafiki wa karibu wa Nyamlani zinaeleza, atachukua
fomu kesho saa 5 asubuhi kugombea nafasi hiyo dhidi ya Jamal Malinzi.
Kabla ya Nyamlani kuchukua fomu, tayari watu wanne wamejitokeza kuwania urais ambao ni Malinzi,
Imani Madega, Wallace Karia na Fredrick Masolwa.
Nyamlani
atakuwa anagombea nafasi hiyo kwa mara ya pili baada ya kugombea kwa
mara ya kwanza na kushindwa na Malinzi ambaye anaonekana kutofanya
vizuri wakati wa miaka yake minne.
Nyamlani
ndiye alikuwa injini ya utendaji wakati wa uongozi wa Leodeger Tenga
ambao ulileta mabadiliko makubwa katika uongozi wa soka nchini.
Post a Comment