Mastaa wafunguka kilichosababisha washindwe Kufutulisha Mwezi Mtukufu
- Staa wa filamu Bongo, Salma Jabu 'Nisha'.
Wakizungumza na gazeti hili hivi karibuni, mastaa mbalimbali walisema kuwa, ni kweli kipindi cha nyuma walikuwa na jeuri ya kufuturisha majumbani kwao, lakini safari hii wamekwama kutokana na kutendwa na JPM aliyekata mirija ya pesa za kiulaini.
- Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
“Kila mmoja amekuwa bahili, kufanya mambo ya kujionesha kama vile kufuturisha, kutuza watu kwenye kumbi za starehe hakuna kabisa, nidhamu ya pesa imeongezeka sana kwa mastaa,” alisema msanii mmoja wa filamu aliyeomba hifadhi ya jina lake ambaye mwaka juzi alifuturisha kwa mbwembwe.
Akaongeza: “Unajua kwa nini nasema Magufuli katutenda vibaya, ni hivi, ukifuatilia sana utabaini kuwa, mastaa wengi hasa wa kike walikuwa wanapata jeuri ya pesa kutoka kwa mapedeshee wao, sasa hivi mapedeshee wamefulia maana serikali imebana mianya ya kupata pesa kirahisi kwa hiyo ‘automatikale’ na mastaa tumefulia.”
Staili mpya ya ufuturishaji
Gazeti hili lilifanya uchunguzi wake na kubaini kuwa, asilimia kubwa ya mastaa wamekuwa wakiandaa futari majumbani kwao na kuwaalika mashosti zao wachache, mazingira yanayoonesha kuwa, zile zama za kufuturisha kwa mbwembwe zimefika mwisho.
- Staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed 'Shilole'.
Aidha, imebainika kuwa, mastaa wengi wa filamu kama vile Wema Sepetu, Kajala, Nisha, Batuli, Lulu na wengineo hawana jeuri ya pesa kama zamani kufuatia kazi zao za filamu kutofanya vizuri sokoni lakini pia mapatna wao waliokuwa wakiwapa pesa za kutesea mjini, wamelosti.
Hali hiyo imewafanya kuwa na pesa ya kuendesha maisha yao peke yao, huku yale matukio ya pati za mara kwa mara, sherehe za kufuru na hata hili la kufuturisha kuonekana ni kama mambo ya anasa.
Wasikie mastaa hawa
Bella: “Kama ni kututenda, kwa kweli Magufuli katutenda vibaya, jeuri ya pesa kwa mastaa wengi sasa hivi kwishnei. Pesa za kutupatupa hakuna tena kama zamani, kila mtu anafuturu kwake na familia yake na si vinginevyo.”
Madaha: “Unajua kuna mastaa waliokuwa wamezoea kufuturisha kama sifa au kujitafutia umaarufu na wengi walikuwa wanafanya hivyo kwa sababu walikuwa wanapata pesa kirahisirahisi, sasa hivi sisi tunaopata pesa za kuungaunga hatuwezi kufanya hayo mambo.
“Wanaofuturisha ni wakubwa tu na viongozi, Magufuli hajamuacha mtu salama, hali ngumu mno, sasa hivi kila mtu anatafuta pesa ili afanye mambo yake ya maana, kuliko kufuturisha umati, mtu anaona bora aende msikitini akatoe sadaka.”
Sikia povu hili:
“Ninachomuomba Magufuli alegeze kidogo, hali ni mbaya sana, tunajua huko tuendako hali inaweza kuja kuwa nzuri lakini daah! Yaani miaka ya nyuma kipindi cha Mwezi Mtukufu nilikuwa nafuturu nyumbani siku chache tu, mara nyingi naalikwa na mastaa wenzangu hasa wa kike kwenda kufuturu lakini safari hii mwezi unaisha sijasikia hata staa anafuturisha, hii inaonesha pesa ya mchezomchezo hakuna, Magu noma kaka,” alisema msanii wa Komedi Jabir Ally ‘Wajajo’.
- Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe.
Sabby Angel: Yaani mambo siyo mambo, ni kweli mwaka jana nilifuturisha lakini safari hii, mhh! Ila bado naweza kufanya hivyo inshaallah!
- Staa wa Bongo Movie, Irene Uwoya.
Wolper: Haya mambo sasa hivi naona hakuna mtu ambaye anaweza kuyaangalia sana, maana maisha ni magumu mno, ujue kila mtu anatafuta jinsi ya kuishika shilingi na si vinginevyo, muhimu ni kuomba dua na kwenda kwa watoto yatima kutoa chochote kitu.
- Staa wa Bongo Movie,Kajala Masanja.
Uwoya: Mimi leo (Jumanne) ndiyo nafuturisha na siwezi kuacha kufanya hivyo hata mara moja, nilikuwa nasubiria tu ya mwishomwisho.
KUTOKA IJUMAA
Gazeti hili linaungana na mastaa waliokuwa na dhamira ya dhati ya kufuturisha lakini linampongeza Rais Magufuli kwa kuleta nidhamu ya pesa kwa walio wengi hasa wale waliokuwa wakitumia pesa zao za kimazabe kufuturisha watu kwa nia ya kujipatia umaarufu.
STORI: MWANDISHI WETU, IJUMAA
Post a Comment