List ya mastaa wa Everton tutakaowaona July 13 inazidi kuongezeka
Everton watakuja Tanzania July 13 2017 kucheza game ya kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya ambao ndio Mabingwa wa SportPesa Super Cup, game hiyo itachezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, uwanja ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 60000.
Dirisha la usajili bado linaendelea na kuelekea maandalizi yao Everton ya msimu mpya wa Ligi Kuu England imeongeza kusajili mastaa wapya ambao tutawaona katika ujio wao July 13, Everton leo June 19 imetangaza kumsajili Davy Klaassen kutoka Ajax na Nathangelo Markelo kwa mkataba wa miaka mitatu.
Post a Comment