Yaya Toure kupewa mkataba mpya Man City
Kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure anakaribia kupata mkataba mpya katika klabu yake anayochezea hivi sasa ya Manchester City.
Toure
alionekana kama hana umuhimu tena klabuni hapo baada ya kuachwa nje
katika kikosi kilichocheza michuano ya Ulaya na hakucheza michuano ya
ligi ya England mpaka mwezi Novemba.Lakini kadri siku zilivyokwenda alianza kuwa na umuhimu klabuni hapo na baadaye kurejea tena kuwa muhimuli wa timu hiyo.
City wataufanya mchezo wa mwisho dhidi ya West Brom kuwa wa kipekee kwa Zabaleta kabla ya kutoa mkono wa kwaheri.
Post a Comment