ad

ad

Yanga Yaipiga Mbeya City Uwanja wa Taifa bao 2-1







FT: YANGA 2-1 MBEYA CITY

Dakika ya 92: Mchezo unaendelea huku kukiwa na presha kubwa kwa pande zote.

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika nne za nyongeza.

Dakika ya 85: Bossou anautoa mpira inakuwa kona. Inapigwa inaokolewa.

Dakika ya 82: Yanga wanapata faulo karibu na kona, inapigwa inaokolewa.

Dakika ya 80: Mchezo unaendelea, Mbeya City wanapata kona, inapigwa Yanga wanaokoa.

Dakika ya 79: Raphael Daudi anapatra nafasi akibaki yeye na kipa baada ya kuwatoka walinzi wa Yanga, anapiga shuti linazuiliwa na Beno, inakuwa kona.


Dakika ya 68: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Nadir Haroub 'Cnnavaro' anaingia Kelvin Yondani. Dakika 67: Kuna vurugu zinatokea kwenye moja ya jukwaa, mashabiki wanapigana, haijajulikana sababu, ila mchezo unaendelea. Baada ya kazi nzuri iliyosababisha kona, Chirwa anaipatia Yanga bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona.
Chirwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO Dakika ya 64: Chirwa anaingia na moira, anawatoka walinzi wawili lakini wa tatu anautoa nje moira inakuwa kona.
A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO Dakika ya 54: Kessy anatoka nje, nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martine. Mashabiki wao wa Yanga wanapiga kelele za kushangilia mabadiliko hayo. Dakika ya 51: Kessy anafika katika lango la Mbeya City lakini anashindwa kuitumia nafasi anayopata, kipa anauwahi mpira anadaka. Dakika ya 51: Kessy anafika katika lango la Mbeya City lakini anashindwa kuitumia nafasi anayopata, kipa anauwahi mpira anadaka. Dakika ya 50: Mwashiuya anaingia na mpira kwa kasi lakini anamsukuma beki wa Mbeya City inakuwa faulo kuelekea kwa Yanga. Dakika ya 48: Niyonzima anapiga krosi nzuri, Tambwe anapiga kichwa kinapaa juu ya lango Dakika ya : 46: Yanga wanafila langoni mwa Mbeya City lakini Tambwe anacheza faulo. Kipindi cha pili kimeanza. Timu zinaingia uwanjani kutoka vyumbani. MAPUMZIKO Dakika ya 48: Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza. Timu zote zinaingia vyumbani kupumzika, Yanga inaongoza kwa bao 1-0. Dakika ya 46: Yanga wanapata kona. Inapigwa na Mwashiuya inatolewa inakuwa kona tena, inapigwa lakini kipa anadaka. Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza. Dakika ya 42: Yanga wanapata faulo nje ya eneo la 18 la Mbeya City baada ya Amiss Tambwe kuchezewa vibaya. Dakika ya 41: Zahoro Pazi anagongana na Bossou ndani ya eneo la 18 la Yanga, Pazi analalamika kuwa amechezewa vibaya. Dakika ya 40: Kessy anapiga krosi lakini beki anazuia mpira unatoka inakuwa kona. Dakika ya 38: Haruna Niyonzima anampa pasi Juma Abdul katikati ya uwanja lakini mpira unatoka nje. Dakika ya 35: Mwamuzi Andrew Shamba anazungumza na wachezaji wa Mbeya City, mchezo unaendelea. Dakika ya 34: Yanga wanafanya shambulizi la kushtukiza, Kessy anakimbia na mpira unaingia lakini unatoka nje. Dakika ya 30: Inapigwa kona lakini Yanga wanatoa tena inakuwa kona. Inapigwa Beno anaupangua mpira na kuelekea katikati ya uwanja. Dakika ya 29: Yanga wanashambuliwa, Kessy anaupiga mpira unatoka nje inakuwa kona. Dakika ya 28: Mbeya City wanapata kona, wanapiga lakini mpira unatoka nje. Dakika ya 27: Mbeya City sasa wanajipanga na kutengeneza mipango ya kushambulia. Dakika ya 25: Mbeya City wamefika langoni kwa Yanga mara mbili na kufanya mashambulizi lakini wameshindwa kutumia nafasi walizopata baada ya kipa Beno kufanya kazi nzuri. Dakika ya 20: Kasi ya mchezo imepungua kiasi. Dakika ya 16: Kwa mara nyingine Yanga wanapata kona, wanapiga kipa anudaka mpira Dakika ya 15: Yanga wanapata kona, anapiga Mwashiuya, mabeki wa Mbaya City wanaokoa. Dakika ya 10: Msuva anashindwa kurejea uwanjani kutokana na kuumia kichwani, nafasi yake inachukuliwa na Juma Abdul Wakati Msuva amevunga bao aligongana kichwani na beki wa Mbeya City, ameshindwa kushangilia, watu wa huduma ya kwanza wameingia kumchukua na kumtoa nje, bado anapatiwa matibabu Dakika ya 8: Yanga wanapata bao la kwanza, krosi nzuri ya Hassana Kessy inatua kichwani mwa Msuva ambaye anapiga kichwa na kufunga.
A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on
Dakika ya 14 yanga wanapata bao GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!! MSUVAAAAAAAA Dakika ya 6: Mchezo umeanza kwa kasi na inavyoonekana timu zote zinataka kupata bao la mapema, Yanga ndiyo ambao wamemiliki mpira muda mwingi. Dakika ya 4: Yanga wanafanya shambulizi kali, Niyonzima anaingia na mpira anapiga krosi lakini inakosa mtu wa kumalizia, mpira unatoka nje Dakika ya 2: Yanga nao wanajibu mapigo kwa kufika langoni mwa Mbeya City baada ya mabeki wa Mbeya kujichanganya lakini mapira unatoka inakuwa kona. Dakika ya 1: Mbeya City wanafika langoni mwa Yanga lakini kipa wa Yanga anauwahi mpira. Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Mbeya City- VPL 1. Beno Kakolanya 2. Hassan Kessy 3. Haji Mwinyi 4. Vicent Bossou 5. Nadir Haroub 6. Thaban Kamusoko 7. Saimoni Msuva 8. Haruna Niyonzima 9. Amisi Tambwe 10. Obrey Chirwa 11. Geofrey Mwashuiya Akiba Deogratius Munishi, Juma Abdul,Kelvin Yondani, Matheo Antony, Deusi Kaseke , Emmanuel Martin na Said Makapu.

No comments

Powered by Blogger.