Video: Maalim Seif atoa rambirambi vifo vya wanafunzi Arusha
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif
Hamadi jana ametoa salam za rambirambi kutokana na vifo vya wanafunzi 29 , walimu
2 na dereva mmoja vilivyotokea Arusha.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi pamoja na Global TV,
Maalim Seif alisema amesikitishwa na vifo hivyo na amewataka wafiwa wote kuwa
na moyo wa subira na akawaombea kwa Mungu waliopoteza maisha.
“Ni wakati ambao inatakiwa serikali iwe wakali kwa madereva
wazembe. Marekani dereva anaogopa kuvunja sheria kutokana na sheria zao kuwa
kali, anapigwa faini za kama dola 300. Kila dereva nchini anatakiwa kuzingatia
sheria za barabarani ili kuepusha ajali kama hizi,” alisema.
Aliwataka polisi wa usalama barabarani kusimamia sheria
ipasavyo ili kuepusha vifo vya ajali kama vilivyotokea Arusha.
Post a Comment