Uzuri, U-Mcharuko, Shepu za Video Queen Vimewabeba Kwenye Vichupa
ILI video ya muziki iwe nzuri zaidi inahitaji wauza sura ‘video queens’ ambao wataibeba.
Tumezoea kuona video nyingi za nje ya Afrika zikiwa na video queen zaidi ya mmoja.
Lakini katika Muziki wa Bongo Fleva zipo video nyingi ambazo kwa asilimia kubwa zinamhusisha video queen mmoja mwenye shepu, mcharuko na hata wengine uzuri wa sura.
Katika makala haya nimekuchambulia baadhi tu ya wauza nyago katika video za Muziki wa Bongo Fleva walioteka katika video walizozifanya kutokana na uzuri, mcharuko na hata shepu zao.
Pia mbali na kufanya video hizo wapo waliojiingiza kwenye muziki ambao wametendea haki uhusika wao.
alisema Mbizo.
Zou
Japo ni mtangazaji wa redio moja nchini lakini kwenye video naye ni muuza nyago wa kiwango. Uzuri na shepu vimechangia kumbeba katika video mbalimbali Bongo. Miongoni mwa video hizo ni Kidebe ya Dogo Janja na Confidence ya TID.
Erycah
Video ya Kwa Hela ya Linex ndiyo imembeba kwa kumpa chati hasa kutokana na uzuri wake. Baada ya hapo amegeuka kuwa gumzo kwenye mitandao hasa picha zake za mitego. Unaweza sema ni mmoja kati ya wauza nyago kwenye video anayeongozwa picha zake kutumiwa katika mitandao mingi ya kijamii kutokana na muonekano wa sura.
Lyinn
Nyota yake ilianza kung’ara katika Video ya Kwetu ya Rayvanny. Katika video hiyo amefanikiwa kuiteka na kuipendezesha kutokana na uzuri aliokuwa nao na mazingira ya video ambayo yalikuwa ya uswahilini.
Kim Nana
Pamoja na kufanya u-modo, Kim naye ni miongoni mwa wauza nyago kwenye video za Kibongo aliyejipatia umaarufu kwenye video kibao ikiwemo Bilima ya Nuh Mziwanda pamoja na Muziki ya Darassa.
Gigy Money
Kama ilivyokuwa kwa Amber Lulu, Gigy naye ni miongoni mwa wauza nyago mcharuko wanaotikisa kwenye video za Kibongo. Mcharuko wake ameuonesha katika video kibao ikiwemo Shika Adabu Yako ya Nay wa Mitego pamoja na ya kwake mwenyewe ya Supu.
Amber Lulu
Licha ya uzuri wake na muonekano wake kufananishwa na mwanamitindo na muuza nyago kutoka Marekani, Amber Rose, huyu ameweza kubebwa na video kibao kutokana na mcharuko wake, miongoni mwa video hizo ni Bongo Bahati Mbaya ya Young Dee, Inde ya Dully pamoja na yake mwenyewe ya Watakoma.
Post a Comment