Taarifa toka BUNGENI kuhusu kukamilika uteuzi wa Wabunge wa CHADEMA Bunge la Afrika Mashariki
1.Tarehe
4 Aprili, 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya
Uchaguzi wa kuwachagua Wajumbe Tisa (9) wa Bunge la Afrika Mashariki
watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge hilo.
Katika Uchaguzi huo, Wajumbe Sita (6) kutoka Chama cha Mapinduzi na
Mjumbe mmoja (1) kutoka Chama cha Wananchi (CUF) walichaguliwa. Wagombea
wawili kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)walikosa kura
za kutosha kuwapatia ushindi.
2.Hivyo,
Bunge linapaswa kufanya uchaguzi kwa mara ya pili ili kuwapata
wawakilishi Wawili (2) kutoka katika Kundi la Vyama vya Upinzani ambapo
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndicho chenye hakiya
kujaza nafasihizo.
3.Katika
mazingira hayo na kwa kuzingatia masharti ya Sheria na Kanuni
zinazotawala Uchaguzi huo, na kwa mamlaka niliyonayo kama Msimamizi
wa Uchaguzi nilitoa TAARIFA ya Siku ya Uteuzi na Siku ya Uchaguzi kwenye Gazeti la Serikali Na. 537 la tarehe 21
Aprili,2017. Taarifa hiyo ilitaja Sikuya Uteuzi(nominationday) wa
Wagombea kuwa ni tarehe 03 Mei, 2017 Saa Kumi Kamili (10:00) Jioni na
Siku ya Uchaguzi(electionday) kuwa nitarehe 10 Mei, 2017.
Hata
hivyo, tarehe 28 Aprili, 2017 Chama cha CHADEMA kiliandikia barua na
kuiwasilisha kwangu siku ya tarehe 2 Mei, 2017 Jioni. Barua hiyo ilitoa
maelezo kwamba muda waliopewa kuwasilisha majina ya wagombea kupitia
kwenye Taarifa hiyo ni finyu kutokana na kuathiriwa na kuwepo kwa siku
za mapumziko ya mwisho wa wiki pamoja na Sikukuu ya Mei Mosi
iliyoanguakia siku ya Jumatatu hivyo, kuwepo kwa ugumu wa kufanya vikao
vyao.
5.Kutokana
na sababu hiyo, Chama hicho kiliomba kuongezewa muda usiopungua wiki
mbili ili kiweze kukamilisha mchakato wa uteuzi wa wagombea, kupata
uthibitisho wa uraia kutoka Idara ya Uhamiaji na uthibitisho wa sifa za
kugombea kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa Ibara ya 50 (2)
ya Mkataba ikisomwa pamoja na Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuriya
Muungano wa Tanzania,1977.
6.Kutokana
na sababu zilizotolewa, niliongeza muda wa siku 4 kuanzia tarehe 3
hadi tarehe 7 Mei, 2017 ili kukiwezesha Chama hicho kukamilisha
taratibu hizo za kisheria na hivyo kukitaka kuwasilisha kwangu
majina na nyaraka za wagombea waliowateua tarehe 8 Mei, 2017 kabla ya
Saa Kumi Kamili (10:00) Jioni ambayo ni Siku ya Uteuzi wa
Wagombea(nomination day).
7.Kupitia
taarifa hii, napenda kuujulisha umma kwamba Chama cha CHADEMA
kimewasilisha kwangu majina sita (6) ya Wagombea wa nafasi mbili za
ujumbe wa Bunge la Afrika Mashariki. Kati ya wagombea hao wanne (4) ni wanaume na wagombea wawili (2) ni wanawake. Majina hayo yamewasilishwa kwangu jana tarehe 8 Mei, 2017 kabla ya mudawaSaa 10 Jionikama nilivyokuwa nimeelekeza.
8.Baada
ya hatua hiyo,nilifanya uchambuzi wa Nyaraka zilizowasilishwa ili
kujiridhisha na uzingatiwaji wa masharti ya uteuzi wa Wagombea kwa
mujibu Ibara ya 50 (2) ya Mkataba, Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, 1977, Kifungu cha 4 (4) cha Sheria ya Uchaguzi wa
Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki na Kanuni 5 (2), (3) na Kanuni ya 6 ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge,ToleolaJanuari,2016.
Matokeo ya uzingatiwaji wa masharti hayo yameainishwa katika Jedwali lifuatalo:
TANBIHI:
√-Maana yake sharti husika limetimizwa
10.Uchambuzi
huo umebainisha kuwa Wagombea wote wamekidhi vigezo na masharti
yanayotakiwa kwa mujibu wa Sheria. Hivyo, napenda kutoa TAARIFA na KUWATANGAZA
wafuatao kuwa Wagombea katika Uchaguzi wa Wajumbe Wawili (2) kupitia
Kundi la Vyama vya Upinzani kutoka Chama cha CHADEMA uliopangwa
kufanyika tarehe10 Mei,2017:
Post a Comment