Shamsa Ford adaiwa KUMFILISI Mume wake
DAR ES SALAAM: Ikiwa ni miezi nane tu imepita tangu aingie kwenye ndoa, staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford anadaiwa kumfilisi mumewe, Rashid Said ‘Chid Mapenzi’, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili. Chanzo makini ambacho ni ndugu wa mume wa Shamsa kililiambia Risasi Jumamosi kuwa mwanamama huyo tangu aolewe, maisha ya Chid Mapenzi yamebadilika kwani hata biashara zake haziendi vizuri jambo ambalo linaonekana kuwa mwanamke huyo amempa gundu. “Kiukweli Shamsa ni kama amempa gundu mumewe kwani tangu waoane mambo siyo mazuri, amekuwa akimkataza kuwa hata na marafiki zake jambo linalowachukiza sana ndugu maana anamrudisha nyuma ndugu yao.
“Angalia mpaka duka walilokuwa nalo pale Mwananyamala-Komakoma wamelifunga na vitu vimerudishwa nyumbani hivyo wanauzia nguo na viatu nyumbani. “Kilichosababisha wakafunga pale ni kwamba kwanza Shamsa anaringa sana pia kodi iliwashinda kwani walitaka kutoa ya miezi mitatu baada ya kodi waliyolipia kuisha hivyo mwenye nyumba akakataa kwani alitaka ya mwaka mzima ndiyo wakaamua kurudisha kwanza nyumbani wakiendelea kutafuta sehemu nyingine,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kujiridhisha, Risasi Jumamosi lilimtafuta Shamsa aliyekiri kuwa ni kweli duka wamefunga lakini wanampango wa kuhamia sehemu nyingine siyo kwamba mumewe amefilisika.
“Nilijua watasema mengi tu lakini ukweli ni kwamba baada ya kuona kodi ni kubwa na biashara ni ngumu nilimshauri mume wangu tuhamie sehemu nyingine na mimi kama mke nina jukumu la kumshauri mume wangu kwa jambo lolote na tumeshapata sehemu nyingine hapohapo Mwananyamala ndiyo tunapafanyia matengenezo tutahamia hivi karibuni tu,” alisema Shamsa.
Post a Comment