ad

ad

Mambo manne ya kufahamu kuelekea fainali ya Simba vs Mbao

Kuelekea fainali ya kombe la FA Cup (Azam Sports Federation Cup) kuna mambo kadhaa ambayo yanainogesha fainali hiyo ambayo itachezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma siku ya Jumamosi Mei 27, 2017.

Fainali hiyo inazikutanisha Simba SC (Dar) na Mbao FC (Mwanza) baada ya timu hizo kuvitoa vigogo vya VPL (Simba wakiitoa Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali huku Mbao wakiivua ubingwa Yanga)

Fainali ya kwanza kuchezwa nje ya Dar

Mkoa wa Dodoma umepata bahati ya kuwa mwenyeji wa fainali ya FA Cup kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa kombe hilo ambapo fainali zote zilizopita zilichezwa Dar. Timu zote zinazocheza fainali zitasafiri kutoka kwenye mikoa yao Simba (Dar) na Mbao (Mwanza) kisha zitakutana katikati ya nchi ambapo pia ni makao makuu ya Tanzania.

Bingwa atasafiri na kombe lake kurejea nalo mkoani kwake, mashabiki watalazimika kusafiri kutoka mikoa mbalimbali kuungana na wale wa mkoa wa Dodoma kuzishangilia timu zao.

Public viewing Centers

Chama cha mpira mkoa wa Dodoma (DOREFA) kimejipanga vizuri kuhakikisha mashabiki watakao kosa nafasi ya kuingia uwanjani (Jamhuri Stadium) wataweza kuishuhudia mechi hiyo kupitia public viewing centers ambazo tayari zimeshaandaliwa huku tiketi hizo za mechi ya fainali hiyo zikianza kuuzwa siku ya Ijumaa siku mmoja kabla ya mechi ili kupunguza msongamano siku ya mechi.

Ushindani wa Mbao

Mbao waliitoa Yanga ambao ndio mabingwa watetezi kwa kuwafunga goli 1-0 katika mchezo wa nusu fainali iliyochezwa CCM Kirumba, Mwanza. Mbao wameweka rekodi katika historia yao katika soka baada ya kupanda ligi na kufika fainali ya kombe la FA msimu huohuo kwa kuwatoa mabingwa watetezi.

Yanga walifungwa pia na Mbao katika mchezo wa mwisho wa ligi kwenye uwanja huohuo wa CCM Kirumba sikuwaliyokabidhiwa ubingwa wao wa VPL huku kwa Mbao ushindi huo ukawabakiza kwenye ligi.

Simba walipata ushindi wa goli 1-0 uwanja wa Uhuru lililofungwa dakika za mwisho kabisa za mchezo huo lakini wakashinda tena mechi ya raundi ya pili kwa magoli 3-2 kwenye uwanja wa CCM Kirumba. Mechi hiyo Mbao walitangulia kuwa mbele kwa magoli 2-0 hadi dakika ya 87 Simba walipoanza kusawazisha na hatimaye kushinda mchezo huo.

Simba

Simba wanaona kombe la FA Cup ndio njia pekee ya kuwafanya washiriki michuano ya kimataifa kwa sababu mshindi wa fainali hiyo atakata tiketi ya mucheza mashindano ya kombe la shirikisho Afrika msimu ujao na kuiwakilisha nchi.

Kjlabu ya Simba haijashiriki michuano ya kimataifa kwa muda mrefu, kwa hiyo mechi ya fainali wanaitolea macho ili kurejesha heshima ya kulitwaa taji hilo litakalowarudisha kwenye anga za kimataifa na pia kutuliza presha ya mashabiki wa klabu hiyo kwa kushindwa kubeba kombe kubwa kwa muda mrefu zaidi ya lile la mapinduzi Cup walilotwaa hivi karibuni.

No comments

Powered by Blogger.