ad

ad

LICHA YA KUCHEMKA KATIKA PREMIER LEAGUE, MANCHESTER UNITED YAIFUNIKA REAL MADRID KWA UTAJIRI

Licha ya kushika nafasi ya sita katika Premier League msimu wa 2016/17, Manchester United imetajwa kuwa ndiyo klabu yenye thamani kubwa zaidi Ulaya ikiifunika Real Madrid.

Utafiti uliofanywa na taasisi ya KPMG imeonyesha kuwa Man United imekuwa na mafanikio makubwa kifedha zaidi ya Real Madrid na Barcelona licha ya kuwa United ina madeni makubwa.
Katika orodha ya klabu zenye thamani kubwa ya kifedha, kuna klabu sita katika 10 bora. Siri kubwa ya United kuongezeka thamani ni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mashabiki sehemu nyingi duniani na kutumia mitandao yao ya kijamii vizuri.
Utafiti huo ulifanyika kwa kutazama mafanikio ya kifedha katika msimu wa 2014/15 na 2015/16.
Bayern Munich inashika nafsi ya nne ikiguatiwa na Manchester City.

KLABU ZENYE THAMANI KUBWA ULAYA
1     Manchester United
2    Real Madrid
3    Barcelona
4    Bayern Munich
5    Manchester City
6    Arsenal
7    Chelsea
8    Liverpool
9    Juventus
10    Tottenham
11    PSG
12    Borussia Dortmund
13    Atlético Madrid
14    Schalke
15    Milan
16    Leicester
17    Everton
18    Roma
19    Inter
20    Napoli
21    Galatasaray
22    Fenerbahce
23    Benfica
24    Lyon
25    Athletic Bilbao
26    Ajax
27    Sevilla
28    Valencia
29    Lazio
30    Besiktas
31    PSV Eindhoven
32    Marseille

No comments

Powered by Blogger.