Karrueche Tran na Chris Brown kutifuana mahakamani
Karrueche Tran atafanya kile ambacho Rihanna hakuweza kufanya – kutoa ushahidi mahakamani kuwa Chris Brown alimkung’uta, na haogopi chochote.
Kwa mujibu wa TMZ, Karrueche yuko tayari kueleza jinsi mpenzi wake huyo wa zamani alivyompiga na kuanguka kwenye ngazi, kumpiga ngumi ya tumboni na kumtishia kumpiga risasi na kumpa vitisho vya kumuua.
Vyanzo vimedai kuwa Karrueche ameamua kusimama kidete ili kuwapa nguvu wanawake wengine ambao wamewahi kupigwa na Breezy kujitokeza na kupaza sauti.
Ripoti zinasema Karrueche alikuwa ameyaficha haya kwa muda mrefu na sasa ameamua kuweka kila kitu hadharani hasa baada ya CB kumtishia kumuua.
Rihanna alikuwa na msimamo tofauti kwa Chris Brown licha ya kupigwa na kujeruhia vibaya na Chris Brown walipokuwa wapenzi, mbapo hakutaka kumshtaki.
Post a Comment