- Mwili wa Ivan ukiwasili kanisani hapo kwa ajili ya kuaga
MWILI
wa aliyekuwa mume wa Zarina Hassan, Ivan Semwanga ambao ulifika Kampala
jana kutoka Afrika Kusini, leo umepelekwa katika Kanisa la Mtakatifu
Paul la Namirembe jijini Kampala kwa ajili ya kupewa heshima za mwisho
kwa ndugu na marafiki.
- Mwili wa marehemu ukiingizwa kanisani
Watu
mbalimbali maarufu walikuwepo kanisani hapo kwa ajili ya ibada maalum,
miongoni mwao akiwemo mfanyabiashara Godfrey Kirumira, Aidah Nantaba, na
Waziri wa Nchi wa Habari na Teknolojia ya Mawasiliano.
Semwanga aliyeacha watoto watatu atazikwa kesho Jumanne nyumbani kwao wilaya ya Kayunga.
- Zari akifunua jeneza lenye mwili wa marehemu mumewe
Semwanga
alifariki katika Hospitali ya Biko Academy iliyoko jijini Pretoria
nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa matatizo ya moyo.
Post a Comment