BAADA YA HANS POPPE, UONGOZI WA SIMBA KUKUTANA NA MO DEWJI
Uongozi wa Simba umepanga kukutana na Mohamed Dewji na kumaliza tofauti zao.
Dewji
maarufu kama Mo, aliamua kujitoa katika suala la mchakato wa mabadiliko
baada ya klabu ya Simba kuingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya
ubashiri ya SportPesa.
Mo
alionyesha kukasirishwa baada ya uongozi kutomshirikisha yeye pamoja na
wajumbe wengine wa kamati ya utendaji, jambo aliloliita kutoaminiana
miongoni mwao.
“Uongozi
utakutana na Mo, itakuwa leo au kesho ili kulimaliza suala hilo.
Kinacholengwa ni kuonyesha busara baada ya matatizo yaliyotokea.
“Kama ambavyo umeona, uongozi umefika kwa Hans Poppe, umekaa na kuzungumza naye na suala limefikiwa kwa kupatikana muafaka.
“Sasa ni lazima kukutana na Mo, Simba hatutaki mifarakano,” kilieleza chanzo.
Post a Comment