RONALDO AMPIGA BAO MESSI, AFIKISHA MABAO 100 LIGI YA MABINGWA ULAYA
Wakati
Lionel Messi alipoingia uwanjani juzi, alikuwa ana mabao 97 aliyofunga
katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mpinzani wake, Cristiano Ronaldo, yeye
alikuwa na mabao 98.
Kila mmoja alitaka kushindana na mwenzake kuwa wa kwanza kuigusa 100.
Barcelona walifungwa mabao 3-0 na Juventus ya Italia, hivyo Messi akabaki na mabao yake 97. Jana ikawa ni zamu ya Ronaldo ambaye amebadilisha namba.
Ronaldo amefunga mabao mawili wakati Real Madrid ikiiangukia Bayern Munich kwao Munich kwa kuichapa mabao 2-1.
Maana yake, Mreno huyo sasa ana mabao 100 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo ameyafunga akiwa na Manchester United na Real Madrid.
Post a Comment