MBAO FC WAANZA KUFANYA UCHUNGUZI KAMA WALIHUJUMIWA VS SIMBA, KIPA ASIMAMISHWA
Mbao FC ilichapwa kwa mabao 3-2 na Simba katika mechi ambayo ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 82.
Taarifa kutoka ndani ya Mbao FC, zinaeleza kipa Eric Ngwengwe amesimamishwa ili kupisha uchunguzi kwa kuwa ni mtuhumiwa.
Makosa mawili ya kipa huyo yalizaa bao la kwanza na la pili la kusawazisha kwa Simba.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza, kipa huyo hajapewa barua ya kusimamishwa zaidi ya kuambiwa kwa mdomo.
Post a Comment