Marouane Fellaini Alambwa Redi, Manchester Derby Ngoma Droo
Baada ya tambo za muda mrefu hatimaye mchezo wa Manchester City na Manchester United umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwenye Uwanja wa Etihad jijini Manchester.
Licha ya kuwa wenyeji Man City ndiyo waliokuwa wakipewa nafasi ya kuopata ushindi mambo yalikuwa magumu na mwisho wa mchezo huo uliomalizika kwa 0-0 ukiwa ni wa nguvu kwa pande zote kutokana na asili ya upinzani wa timu husika ambapo zinapokutana mchezo wa unatambulika kwa jina la Manchester Derby.
Mchezo huo ambao ulionekana kutawaliwa na mbinu kali za makocha hao hasa katika safu ya kiungo ulikuwa na kasi na kwa matokeo hayo sasa zote zimebaki katika nafasi zilizomo kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’.
Man City imebaki nafasi ya nne ikiwa na pointi 65 wakati United imebaki nafasi ya tano ikiwa na pointi 64, zote zikiwa zimesaliwa na michezo mitano kumaliza msimu huu wa 2016/17.
Walikuwa ni Man City ndiyo ambao walionekana kutawala lango la wapinzani wao mara nyingi kuanzia kipindi cha kwanza ambapo United walionekana kuwa vizuri kwenye safu ya ulinzi.
Straika wa Man City, Sergio Agüero alipiga mashuti kadhaa lakini yote yalitoka nje ya lango au kudakwa na kipa David de Gea.
Kiungo wa Man United, Ander Herrera aliingia kwenye mzozo mara kadhaa na viungo wa Man City, Fernandinho na Yaya Toure.
Kipa wa Man City, Claudio Bravo aliumia mkono na kutolewa katika dakika ya 79 nafasi yake ikachukuliwa na Wilfredo Caballero.
Post a Comment