ad

ad

MAN UNITED YAANZA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE KWA KUSUASUA, YALAZIMISHWA SARE UBELGIJI



Man United imeshindwa kutamba katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Europa League baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Anderlecht ya Ubelgiji.

Maana yake, Man United itaitegemea mechi yake ya pili itakapokuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester.

Henrikh Mkhitaryan ndiye aliyefunga bao la Manchester United ambayo itajilaumu kupoteza nafasi nyingi zaidi za kufunga.

Wakati ikionekana kama Man United wameshinda, Leander Dendoncker alisawazisha katika dakika ya 86 na kumaliza furaha ya Kocha Jose Mourinho.


Man United starting XI: Romero, Valencia, Bailly, Rojo, Darmian, Carrick (C), Pogba, Mkhitaryan, Lingard, Rashford, Ibrahimovic 
Subs: De Gea, Blind, Fosu-Mensah, Shaw, Fellaini, Herrera, Martial










No comments

Powered by Blogger.