KIATU CHA HIMID MAO, KIMEMJERUHI ZULU VIBAYA, KURUDI LABDA ZAIDI YA WIKI TATU BAADAYE
Kiungo
Mzambia, Justine Zulu alilazimika kutoka nje na nafarsi yake
kuchukuliwa na Emmanuel Martin baada ya kukumbana na kiatu cha nahodha
wa Azam FC, Himid Mao.
Yanga imeitwanga Azam FC kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Awali
ilionekana kama mzaha, lakini Zulu ameshonwa zaidi ya nyuzi tatu na
imeelezwa huenda itachukua kuanzia wiki mbili hadi mwezi kwake kurejea
tena uwanjani.
Hata hivyo, mmoja wa wauguzi waliomchukua kumtoa nje, amesema inawezekana akapona haraka.
Zulu alipiga shuti na Himid akaingiza mguu, iinaonekana kiatu ndiyo kilichomjeruhi.
Post a Comment