FAKHI AENDELEA KUSISITIZA KUWA HANA KADI YA TATU YA NJANO
Beki Mohamed Fakhi, ameendelea kusisitiza kwamba hana kadi ya tatu ya njano kama ilivyoelezwa na Kamati ya Saa 72.
"Sina kadi ya tatu, nina uhakika na rekodi zetu ndiyo ziko sawa," amesema Fakhi.
"Hivyo
ninajiamini kuwa sikuwa na kadi," alisema Fakhi mara tu baada ya
kumaliza kuhojiwa na Kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Post a Comment