Edo Kumwembe Aichana Yanga kisa kuomba ichangiwe pesa
Jumatatu ya April 24 klabu ya Yanga ilizindua mpango wa kuomba mashabiki na wanachama kuichangia timu yao ili kuiwezesha kiuchumi, kila mmoja anafikiria wazo lake lakini moja kati ya watu ambao wamelipokea kwa utofauti ni mchambuzi mahiri wa habari za michezo wa Gazeti la MwanaSpoti Edo Kumwembe.
Haya ni mawazo ya Edo Kumwembe kupitia ukurasa wake wa facebook kuhusiana na suala la Yanga kuomba ichangiwe kwa njia ya simu na mashabiki wake.
“Yanga inaomba mchango kwa mashabiki wake? What a shame…mchango wa mashabiki wa Yanga ni kununua jezi original za timu na bidhaa kedekede zinazoambatana na jina lao. Mmewapelekea? Hapana. Mchango wa mashabiki wa Yanga ni kwenda kwa wingi viwanjani timu yao inapocheza ili wadhamini wajue ukubwa wa Yanga waipapatikie”
“Ni kweli mashabiki wanajitokeza na wadhamini wanaitamani Yanga, mdosi anabana ili aabudiwe, kamuulizeni jinsi Tiboroha alivyotimuliwa na mipango yake…kwa kuipenda Yanga tu kwa wingi wao tayari ni mchango tosha…walihitaji viongozi wa kutumia fursa hiyo Yanga iwe matawi ya juu san
Post a Comment