Yusuf Manji Mahakamani Tena Kesho
Kesi
inayomhusu Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ya juu ya matumizi ya dawa
za kulevya aina ya Heroine, inatarajiwa kusikilizwa tena kesho Alhamisi
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuahirishwa kwa mara ya
mwisho Februari 16, mwaka huu.
Manji
anatuhumiwa kutumia madawa hayo kinyume na sheria ya mwaka 2015 ya
kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya kifungu cha 17 (1) namba 5
ambapo inadaiwa Manji alitumia dawa hizo Februari 6 na 9, mwaka huu.
Kesi
hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha huku upande
wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Osward Tibaloyekomya huku upande wa
Manji ukiongozwa na Wakili Alex Mgongolwa.
Baada
ya kusikilizwa kwa mara ya kwanza kwa kesi hiyo, Manji alikataa
mashtaka hayo na kuachiwa nje kwa dhamana ya milioni 10 iliyotolewa na
Katibu wa Yanga, Charles Mkwasa.
Lakini
kuna uwezekano mkubwa wa kusikilizwa kwa kesi hiyo bila ya Manji kuwepo
kutokana na kuumwa kwani kwa sasa amelazwa kwenye Hospitali ya Aga Khan
ambapo anasumbuliwa na tatizo la moyo.
Post a Comment