Wafanyakazi 9 wa TBC wasimamishwa kazi kwa kutangaza habari ya uongo kuhusu Rais Magufuli
Wafanyakazi
tisa wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wamechukuliwa hatua za
kinidhamu kufuatia kurusha habari ya uongo kuhusu Rais Dkt John Pombe
Magufuli.
Wafanyakazi
hao wamesimamishwa kazi kufuatia kurusha taarifa ya uongo kutoka tovuti
ya fox-channel.com ambayo ilidai kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump
amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa utendaji wake mkubwa na
vita dhidi ya dawa za kulevya. Tovuti halali ya Fox ni foxnews.com na si
hiyo iliyonukuliwa na TBC.
Mkurugenzi
wa TBC, Dk. Ayoub Riyoba amethibitisha kuchukuliwa kwa hatua za
kinidhamu kwa wafanyakazi hao kufuatia kosa hilo walilolifanya.
“Ni kweli watu kadhaa wamesimamishwa kazi kutokana na suala hilo.”
Post a Comment