SIMBA KUTOFANYA UTANI DODOMA, WAMEPANGA KUSHUKA FULL "MKOKO"
Vinara
wa Ligi Kuu Bara, Simba, leo wanacheza mechi ya kirafiki dhidi ya
Polisi Dom iliyopo Ligi Daraja la Kwanza lakini wakali hao wa Msimbazi
wamesema wala hawatadharau mchezo huo na wamepanga kushusha kikosi cha
kwanza.
Ligi
Kuu sasa hivi ipo kwenye mapumziko kupisha michuano ya Kombe la FA
pamoja na michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la
Shirikisho Afrika ambapo Yanga na Azam zinashiriki.
Mchezo
huo utapigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Ikumbukwe katika
mchezo wa mwisho uliozikutanisha timu hizo, Simba ilipata ushindi wa
mabao 2-0 ambapo ulipigwa uwanjani hapo Septemba 3, mwaka jana katika
mechi iliyoandaliwa na uongozi wa chama cha soka mkoani humo. Mabao ya
Simba yalifungwa na Abdi Banda na Said Ndemla.
Kocha
Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja amesema wamejipanga vilivyo
kwa ajili ya mchezo huo na wanauchukulia kama sehemu ya maandalizi ya
mchezo wao wa Kombe la FA dhidi ya Madini FC ya Arusha utakaopigwa Machi
19, mwaka huu.
“Tumejipanga
vizuri kwa ajili ya mechi hiyo ambayo ni muhimu kwetu kwa ajili ya
kujiweka sawa na mechi yetu ya robo fainali ya Kombe FA, hivyo tutaingia
uwanjani kwa ajili ya kupambana na kuhakikisha tunaibuka na ushindi.
“Lakini
pia tunataka kuendeleza rekodi yetu ya kufanya vizuri mkoani hapa, tena
dhidi ya Polisi Dodoma ambapo mwaka jana tuliifunga mabao 2-0 katika
mchezo wetu wa kirafiki, hivyo nitumie nafasi hii kuwataka wapenzi na
mashabiki wa timu zote mbili kujitokeza kwa wingi ili waje wapate
burudani ya soka la kuvutia,” alisema Mayanja.

Post a Comment